Wahitaji wa mikopo wenye vipaumbele na hawakupata mkopo, fika bila ya kukosa


WIZARA YA MIKOPO IFMSO

Kwa wanafunzi wa IFM wote wanaoendelea na hata wale mwaka wa kwanza wote ambao hakupata mikopo kutoka bodi ya mikopo elimu ya juu Tanzania na wanavigezo mfano: Yatima ama una mzazi mmoja na hujiwezi kiuchumi.
Pia wanafunzi wa Mwaka wa kwanza waliotokea diploma na wanahitaji msaada kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na inawapelekea kutomudu gharama za kujiendeleza kimasomo katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM.

Wizara ya mikopo IFMSO inawatangazia kuwa wafike kesho katika ofisi za ifmso kuanzia saa tano asubuhi (11:00) wajiandikishe majina yao wizara ya Mikopo kushirikiana na serekali ya wanafunzi (IFMSO) itatia juhudi kupata ufadhili kutoka bodi ya mikopo HESLB, ni zoezi la siku moja fika bila kukosa.

Hata kama uliwahi kuandika taarifa zako IFM-SO tunaomba ufike uandike tena taarifa hizo. Samahani kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imeandaliwa na W/Mikopo IFMSO
Patrick Steven James (+255 712 658869)
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment