MAHITAJI YA HOSTEL AU VYUMBA NJE YA CHUO
Ndg, Wanafunzi wa chuo cha usimamizi fedha. Poleni Na maandalzi ya Mitihani ya mwisho wa semester.
1. Wizara ya mambo ya nje , inapenda kuwatarifu wanafunzi ambao watahitaji kutafutiwa chumba au hostel kwa kipindi cha likizo fupi kuanzia tarehe 24 /02/2017 mpaka 13/03/2017.
Kwa ambao watahitaji
Mnatakiwa kuja kuandika majina yenu na taarifa zingine muhimu kwenye fomu za OCM zilizopo IFMSO -312. Mpaka sasa OCM imehudumia zaidi ya wanafunzi 450 na huduma hii ni bureee.
2. Wizara ya mambo ya nje inapenda kuwashukuru wawakilishi wa madarasa na wanafunzi wote walioandikisha majina yao kwenye off campus students form. ( lengo kuu la kuandikisha majina hayo ilikuwa ni kupata idadi kamili ya wanafunzi ambayo ingepelekea wizara kufika mamlaka husika na kuomba baadhi ya majengo posta tuyatumie kama hostel).
Lakin idadi kamili ya off campus students iliyopo kwa waziri wa mambo ya nje mpaka sasa ni wanafunzi 1679 kwa stream 25 Kigamboni ikiwa na off campus students zaidi ya 1283.
3. Wizara ya mambo ya nje inawaomba wanafunzi wa IFM wakazi wa Kigamboni (ferry, tuamoyo, Tungi, muungano na Magogoni) tuliowaombea ruhusa ya kwenda kusomea MNMA, wawe watulivu na waskivu kwa walinzi wa chuo cha mwalimu nyerere .kwa sababu taarifa tunazopatiwa hazifurahishi. Nenda na kitambulisho chako cha chuo na tafadhali, fuata utaratibu utakao ukuta.
4. Mwisho wizara ya mambo ya nje.inawaomba wanafunzi kutumia product yetu ya IFM- SO. Kama wizara tunamiliki application ambayo imerahisisha mambo na kuweka huduma ya utaftaji wa vyumba na hostel wa kidigitali zaidi, inakurahisishia kupata vyumba au hostel kupitia simu yako ya kiganjani. Install dalaliAppTz kutoka google play store. Kisha log in kama client, Utaona Nyumba na hostel ambazo ziko uploaded. Room Na hostel zinapatikana.
IFMSO 2016/2017
Wizara ya mambo ya nje
Serikali ya wanafunzi IFM-SO inawatakia maandalizi mema ya mitihani ya mwisho. Mungu awe nanyi kwenye maandalizi yenu, awafanyie wepesi mitihani yenu na kwa pamoja tufaulu kwa alama nzuri.
Naulizia hostel za nje jiran na IFM
ReplyDeleteNaomba kujua kama umepata Hostel ama laa. Na tunaomba sana radhi kwa kuchelewa kujibu comment yako.
DeleteHostel
ReplyDelete