Ufafanuzi wa status zinazoonekana kwenye matokeo ya wanafunzi


TAARIFA INAYOTOA UFAFANUZI WA STATUS ZINAZOONEKANA
KWENYE MATOKEO YA WANAFUNZI

SUPPLIMENTARY:
Mwongozo kwa wanafunzi wanaotakiwa kufanya mitihani ya supplimentary

1.       Mwanafunzi anahitajika kufanya mtihani wa supplimentary baada ya matokeo ya semista ya pili.

2.       Wanafunzi wote (Undergraduate na Postgraduate) ambaye amefeli mtihani wake, anaruhusiwa kufanya mtihani wa supplimetary ikiwa hakufeli zaidi ya nusu ya masomo yake kwa semista. Mfano: Mwanafunzi mwenye kozi 6 (Masomo 6) asifeli zaidi ya masomo matatu (3).

3.       Mwanafunzi atakaefanya mitihani ya supplimentary, maksi zake za Course work hazitatumika kwenye kutoa matokeo yake ya supplementary.

REPEAT A YEAR:
Mwongozo kwa wanafunzi wanaotakiwa kurudia mwaka.

1.       Kwa mwanafunzi wa Degree au Diploma anaruhusiwa kurudia mwaka husika endapo amefeli nusu ya masomo yake kwa mwaka.

2.       Mwanafunzi akifeli zaidi ya nusu ya masomo yake kwa semista ya kwanza kwa mwaka wa masomo, anaruhusiwa kurudia mwaka. (Sheria hii haiwahusishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza).
-          ZINGATIA:
1.       Kwa taarifa zaidi, soma “examination regulation” ndani ya prospectus ukurasa wa 24, na kwenye akaunti ya kila mwanafunzi (SIS) ukurasa wa 22.

2.       Kwa masharti ya mitihani ya supplimentary, soma kifungu nambari 19(1-4), ukurasa 242 (Prospectus) na 23- PDF kutoka kwenye (SIS).

3.       Kwa masharti ya wanaorudia mwaka, soma kifungu nambari 21 (a-f), ukurasa 246 (Prospectus) na 23 PDF kwa watakaoipakua kutoka kwenye akaunti ya (SIS).


4.       Kutokana na taarifa tajwa hapo juu, STATUS ZA WANAFUNZI ZIKO SAWA. Mfano: Kama umeandikiwa “SUPP” utafanya supplimentary zako, kama “REPEAT” utarudia mwaka.






IFM-SO 
2016/17
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment