Kutoka wizara ya mikopo IFM-SO



 TAARIFA KWA WANUFAIKA WA MIKOPO CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

OFISI YA MIKOPO CHINI YA OFISI YA SERIKALI YA WANAFUNZI IFMSO INAPENDA KUTOA TAARIFA JUU YA UTARATIBU WA UTOAJI WA FEDHA ZA KUJIKIMU KATIKA MAFUNZO YA VITENDO (FIELD)

Pesa za field zitasainiwa na wanafunzi kabla ya kuingizwa katika account za wanafunzi kwa mujibu wa muongozo wa wizara ya elimu, serikali ya wanafunzi imelifuatilia kwa ukaribu zaidi kutetea maslahi ya wanafunzi kama taarifa iliyotolewa awali na ifmso, lakini kutokana na sababu hizo zilizo ainishwa na muongozo kutoka wizara ya elimu ikiwamo kupunguza risk zitakazojitokeza [wanafunzi kufeli {disco} watakao hairisha mwaka wa masomo na kupelekea kutofika chuoni kusaini endapo pesa zitatolewa bila kusaini.

Fedha ya mafunzo itaingizwa kwa awamu mbili wiki nne za kwanza pia wiki nne zitafuata zote zitakuwa na utaratibu maalumu na serikali ya wanafunzi itatoa utaratibu mzuri.

Serikali ya wanafunzi katika majadiliano ya mwisho na uongozi wa chuo imefikia maamuzi ya kuwaomba wanafunzi kujitahidi kusaini fedha hizo mapema iwezekanavyo bila kukosa kupunguza matatizo ya aina yoyote.
HALI YA KILA MWANAFUNZI ITAZINGATIWA.

IMETOLEWA NA
WIZARA YA MIKOPO
(IFMSO)



Share on Google Plus

About UPStream Telecom

3 comments:

  1. Hamuwezi kuwa hamjalewa IFM-SO na hamko kwa maslahi ya wanafunzi ila maslahi yenu,UD na ARDHI wameyawezaje hayo,kasomeni ata tuition kwao basi

    ReplyDelete
  2. So me ningeomba kiongozi wa mikopo kupitia wizara yako husika chin ya IFM-SO utupe majib ni lini fedha zetu zitakuwa zimewekwa kwwnye account ?

    ReplyDelete
  3. Eewe waziri wa mikopo... lini hiyo hawamu ya pili tutapewa pesa zetu hapa IFM.. na tunaomba tufahamu tatizo ni body ya mikopo wamechelewesha awamu ya kwanza au ni IFM wamechelewesha kutulipa ili tufahamu kwetu awamu ya pili ni week ijayo au mwezi ujao

    ReplyDelete