Ulinzi unaanzia kwangu na kwako, tulinde mali zetu, tuishi salama


ULINZI UNAANZIA KWANGU NA KWAKO, TULINDE MALI ZETU, TUISHI SALAMA


Wizara ya mambo ya nje na wizara ya mambo ya ndani ( off campus ministry @ Ministry of campus) inakemea vikali vitendo vyote viovu vinavyofanyika katika jamii zetu za nje na ndani ya chuo.
Vitendo hivyo ni  kama i)  kuibiwa na 
                                      ii) kuiba au kushirikiana na wahalifu kuiba mali ya mwanachuo mwenzako.

Wizara ya mambo ya nje inakumbana na changamoto kuhusu suala la ulinzi na usalama wa wanafunzi wanapokuwepo nje ya chuo.

Kumekuwa na matukio mbalimbali ya wizi ambayo yanafanyika katika jamii ya (Kigamboni, magomeni na kinondoni) na matukio haya husababishwa mara nyingine na mwanafunzi binafsi. 

Nini Kifanyike?
.
1. Mwanachuo hakikisha ukiwa umetoka chuo (Kuanzia saa mbili usiku na kuendelea) na umebeba vitu vya thamani kama laptop, simu, na kadhalika, jitahidi usitembee peke yako, na jihadhari kwa  kutopita njia usiyoijua na njia za vichochoroni.

2. Kwa wanachuo wote wanaokaa hostel za nje, mfano ndani ya hostel mnaishi wanafunzi zaidi ya 10 na kuendelea, jiwekeeni  desturi ya  kila  mgeni anayeingia hostel kwenu awe anatambulika kuwa ni mgeni wa nani,   na ikiwezekana  mwenye mgeni atambue tabia  ya mgeni wake.( lengo ni  kuepusha wizi unaofanywa na vibaka kwa kuigiza kuwa ni  mgeni wa mwanachuo ndani ya hostel.)

3. Kwa wanachuo wanao kaa kwenye vyumba vya kupanga, Hakikisha hauweki vitu vya thamani kwenye madirisha yenu au sehemu inayoonekana kirahisi, pia  kumbuka kuweka mapazia na ikiwezekana gongea mabox kwa ndani  ili hata kibaka akitaka kuchana dirisha lako imuwie  ugumu. Pia kumbuka kutambua tabia za majirani zako. Funga mlango wako kila unapotoka, (hata kama unaenda chooni) na usimuamini kila mtu kwa usalama wako na mali zako. 

4. Kwa wanafunzi wanaoishi hostel na vyumba vya kupanga, unapomuona mtu yeyote unemtilia shaka na usiemjua, usisite kumhoji na ikiwezekana kwa usalama zaidi umsindikize mpaka katika chumba cha mtu aliesema anamfuata. kama atakuwa ni mtu wa shari, toa taarifa kwa kiongozi wa hostel, mwenye nyumba au marafiki zako ili muweze kumkabili mtu huyo.

5. Wizara imepokea malalamiko kutoka maeneo kadhaa wanayokaa wanafunzi wenzetu kwa kuongoza kuwa na matukio ya vibaka kupora simu na uchanaji wa madirisha. Kwa pamoja tujitahidi kufuata njia za kujihami na kutunza mali zetu tajwa hapo juu na kuweka mali zetu vizuri, kwani  mwizi anaweza akawa ni rafiki yako, jirani au jamii inayokuzunguka. Maeneo hayo ni:
  • Big brother 
  • Midizini
  • Kwa urasa
  • Serengeti.

Hatua iliyochukuliwa:

Wizara ya mambo ya nje imereport matatizo haya kwa mamlaka husika ya ulinzi na usalama, kituo cha polisi Kigamboni.

Na mkuu wa kituo cha polisi kigamboni ameahidi kuyafanyia kazi maeneo tajwa hapo juu, pia akishauri wanavyuo tuwe walinzi wa kwanza wa kutunza mali zetu na za wenzetu.

"Wizara ya mambo ya nje inaendelea kufuatilia usalama wa kila mwanafunzi wa IFM anaeishi nje ya chuo ili kuboresha amani katika maisha yake yote ya masomo chuoni, na inasisitiza wanafunzi wasiojisajili kwenye off-campus forms, wajisajili, ili kurahisisha ufuatiliaji wa haki za wanafunzi wenzetu kwa kuwa na takwimu zao"
  
IFM-SO 2016/17
wizara ya mambo ya nje.
Tunawatakia mitihani mema.
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment