Katazo la maandamano na makubaliano na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni


KATAZO LA MAANDAMANO YA AMANI KUTOKA OFISI YA MKUU WA POLISI WILAYA YA KIGAMBONI

Kufuatia barua iliyotumwa na serikali ya wanafunzi ya tarehe 17/03/2017 kuhusu taarifa ya maandamano ya amani. 

Jana tarehe 20/3/2017 saa 2 usiku, ilipokelewa barua kutoka ofisi ya mkuu wa polisi Wilaya ya Kigamboni ikihusu KATAZO, yenye kumbukumbu namba KGD/C.13/26. Ofisi ya mkuu wa polisi imekataza kufanyika maandamano hayo ya amani (yaliyokuwa yafanyike kesho, 22/3/2017) kwa kunukuu vifungu vya sheria K/F 43 (4), 44, 45 na 46 (2) (b) cha sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi sura ya 322 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 (R.E 2002).

Hatua zilizochukuliwa na serikali ya wanafunzi IFM
Baada tu ya kupokea barua ya katazo hilo, serikali ya wanafunzi imefanya mawasiliano na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kigamboni na leo (21/3/2017) asubuhi, Serikali ya wanafunzi ikifuatana na ofisi ya Mlezi wa wanafunzi ilikutana na mkuu wa wilaya ya kigamboni.

Yaloyokubaliwa kwenye kikao
1. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi (Mkuu wa wilaya) ametoa ahadi ya kushirikiana na vyombo vya usalama, OCD, na wenyekiti wa serikali za mitaa wilaya ya kigamboni kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi kwa kila serikali ya mtaa pamoja na kuongeza polisi wa doria ili kuimarisha ulinzi katika wilaya hiyo.

2. Serikali ya wanafunzi imekubaliana na mkuu wa wilaya kufanyika kwa kikao baina ya wanafunzi na kamati ya ulinzi wilaya (Mkuu wa wilaya, OCD, Madiwani, Afsa mtendaji kata, na Wenyeviti wa serikali za mitaa) kujadili hatma ya usalama wa wanafunzi na wanajamii waishio kigamboni na kupata majibu ya kero za wanafunzi wa Kigamboni.

3. Mkuu wa wilaya ameahidi kutupa ushirikiano punde tu tutakapomuhitaji, na yeye pia ameomba kupewa ushirikiano wa wanafunzi endapo atahitaji ushirikiano wetu.


NB: Serikali ya wanafunzi itatoa taarifa juu ya siku ya kikao na mkuu wa wilaya na serikali inasisitiza mahudhurio ya wanafunzi kwa wingi katika kikao hicho kwani kwa sasa ndipo mahali pekee tunaweza kufikisha kero zetu na zikafanyiwa kazi.

  • Wanafunzi wafike chuoni, masomo yanaendelea kama kawaida
Serikali ya wanafunzi
IFM-SO 2016/17




  

Share on Google Plus

About UPStream Telecom

2 comments:

  1. binafsi nashukuru kusikia hivyo ila ninaomba tarehe ya kukutana na ofisiya mkuu wa wilaya ya Kigamboni itanjwe mapema kwa sababi ziguatazo
    1:kila siku matatizo yanazidi huku kigamboni dhidi ya wanafunzi
    2:kuandaa au kujiandaa kero za ufasaa yani bila kupurukushwa
    3:kuwa na mazingira mazuli ambayo hayawezi kumsababisha mwanafunzi kufeli au kuumia kimasomo.
    4:Mr president naomba nilioyanena hapo juu kwa maandishi uyaangalia kwa jicho moja bila kuleta utetesi wowote ule
    5:mwisho naomba wanachuo wenzangu tuwe na ushirikiano bindi tunapoitajika sehemu furani

    ReplyDelete