Makubaliano ya kikao na registrar kwa maslahi ya wanafunzi wa IFM


YALIYOJADILIWA NA MAKUBALIANO YA KIKAO CHA TAREHE 7/1/2017 NA REGISTRAR

Wizara ya elimu IFMSO inapenda kuwataarifu wale wote ambao hawajafanikiwa kufanya registration kuwa jana 6th January 2017 tulikaa kikao pamoja na registrar na baadhi ya wanafunzi ambao hawajafanya registration na mambo yafuatayo yalikubaliwa:

1. Wanafunzi ambao wameshindwa kufanya registration kwa kigezo cha kukosa ada wamepewa grace period ya siku 10 mpaka siku test 2 itakapoanza yaani 16th January 2017 kuweza kukamilisha kiasi kinachohitajika ili waweze kufanyiwa usajili.

2. Wanafunzi wametakiwa wajiassess wenyewe na wale ambao wanaona kwamba hawataweza kabisa kufanikisha kiasi cha hela stahiki wamesihiwa kuahirisha mwaka wa masomo kwa kuandika barua inayoeleza sababu za kufanya hivyo kwa dean of faculty husika, hakikisha umepata barua ya mrejesho kutoka kwa dean of faculty ambayo utaitumia mwakani unapokuja kufanya usajili, failure to do so itapelekea status yako kuwa abscond & discontinued.

3. Iwapo mwanafunzi alikuwa amelipia kiasi cha ada na ameshindwa kumalizia ili aweze kusajiliwa, atakapo andika barua ya kuahirisha mwaka kwenda kwa dean of faculty aweke wazi kuwa kuna kiasi alilipia na aambatanishe na COPY ya risiti ya malipo na ahakikishe kwenye barua ya mrejesho kutoka kwa dean of faculty suala hilo limekuwa noted clearly ili kiasi hicho kiwe carried forward atakapokuja mwaka wa masomo unaofuata aweze kukitumia hicho hicho.

4. Wale wanufaika wa mikopo waliotumia commitment forms kufanikisha malipo ya ada na bado hawajasajiliwa wametakiwa kuingia kwenye system mara kwa mara kucheki kama wamekuwa registered.

5. Wale wanufaika wa mikopo ambao walikua na matatizo kama incomplete katika matokeo yao ya semester iliyopita na hivyo kusababisha allocation zao kuchelewa wametakiwa kumuona REGISTRAR office namba D11 (block D) ili waweze kusaidiwa.

6. Wale ambao walitumia commitment forms ila kuna kiasi walitakiwa kutop up ambacho wamelipia/watalipia ila bado hawajafanyiwa usajili pia wametakiwa kumuona Registrar waweze kupewa msaada zaidi.

NB:
PINDI UTAKAPO LIPA HIYO ADA, ANDIKA BARUA YA KUOMBA KUFANYIWA USAJILI KWENDA KWA OFISI YA REGISTRAR, BARUA HIYO HAITAJIBIWA BALI NDANI YA SIKU MBILI UTAFANYIWA USAJILI AUTOMATICALLY. UKISHAKUWA REGISTERED FIKA PALE ADMISSION WAAMBIE UMEFANYA USAJILI NDANI YA SIKU KADHAA ZILIZOPITA *(USIDANGANYE)* ILI UWEZE KUPATA KITAMBULISHO CHAKO KWA URAHISI.

*WOTE AMBAO HAMJASAJILIWA MNATAKIWA MUWE MMEANDIKWA KWENYE ORODHA ITAKAYOPELEKWA KWA REGISTRAR JUMATATU. KAMA UNAJIJUA HAUJAANDIKWA JINA LAKO TAFADHALI TUMA REG. NUMBER YAKO NA JINA LAKO KWENDA KWENYE NAMBA 0712812737 (KATIBU WIZARA YA ELIMU) ILI UWEZE KUANDIKWA. MWANAFUNZI AMBAYE HATAKUWA KWENYE HIYO ORODHA HATASAIDIWA KWA NAMNA YOYOTE NA REGISTRAR.* 

 WIZARA YA ELIMU IFMSO
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment