Tangazo
Ufadhili Maalum Elimu kwa Wasichana Tu: 2016-2025
Chini ya Ufadhili wa Marafiki Bora wa Mama na Elimu Kwa Mtoto wa Kike [The
Good Friends of Mothers and Girls Education]. Uhai Tanzania ni shirika
la Afya ya Umma, lililoanzishwa lililosajiliwa 01.07.2011 kwa Na.84286 chini ya
sheria za Mashirika ya Brela. Kwa sasa linafanya kazi ya Kuzuia vifo vya Uzazi
kwa Wanawake Wajawazito, kwa kupitia kutoa elimu ya masomo ya darasani [fomrla
education] Kwa wasichana tu.
Shirika linapenda kuwatangazia makundi haya [1] Wasichana ndani ya jamii [Umma] na [2] wanawake
na wanaume wanafunzi wa kawaida-madarasa ya Kiingereza, Elimu ya masomo ya
Sayansi, Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma, Eosiolojia [Sociology], na [3] wanawake na wanaume viongozi wanaotaka kufadhiliwa kuomba Ufadhi
Maalum Kwa masomo ya Mwaka wa Masomo 2017 tu. Pia Shirika linawahimiza wazazi
nchini Tanzania, Afrika na Duniani kuwawezesha
Wasichana, watoto wao wa Kike wanaotaka kufadhiliwa Masomo kuomba.
Tangazo hili ni kwa nafasi za Umma kwa ujumbla na sio chuo au jamii fulani.
Wanafunzi chini ya Programu hii ya Ufadhili watasoma katika shule
zifuatazo: Makongo, Jangwani, Zanaki, Morogoro, Dar es Salaam Baptist, Ubungo Modern, Loyola, na Educare. Shule za Msinigi ni Grace [Sinza],
Atlas [ Ubungo], Sunrize [Mikocheni], Vyuo vikuu ni Chuo Kikuu cha Dar es
salaam, SUA, Chuo Kikuu cha Tiba Shirikishi [Muhimbili], Chuo Kikuuu cha Ardhi,
na nyuo vikuu vya nje ya Tanzania-ndani ya Africa na Ulaya.
Masomo ya:
Ngazi za masomo ni Chekechea, Msingi na /Kozi Maalum ya Kiingereza, Kurudia Mitihani, QT,
na masomo ya O level, A level, na masomo ya QT, Vyuo vya Ufundi, Utalii,
Ujasiriamali, na Vyuo Vikuu.
Huduma
za Ufadhili: Ufadhili utatoa Ada ya masomo [Karo],
Usafiri wa kwenda na kurudi nyumbani wakati wa likizo, vifaa vya darasani, vitabu
vya mwanafunzi mwenyewe, kula, Bweni, malazi, matunzo ya muhimu kwa msichana.
Masharti
ya Jinsi ya kuandika na kutuma barua ya Maombi
Wasichana na wanawake, na wanaume waandike barua ya Mkono ya Kiswahili [isichapishwe]
aitume kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji Uhai Tanzania, S.L.P 70913,Dar
es Salaam, na au kukusanya katika semina na shughuli zetu Kila jumapili Ubungo
Dar es salaam [piga simu kujua]: Wazazi wa watoto wa Chekechea waandikie
barua watoto wao.
Ada
ya Maombi isiyorudishwa:
·
Maombi ya Chekechea: Tsh 15,000=; Maombi ya Msingi na O level: Tsh 15,000/=;
·
Maombi ya Kidato cha 5, Vyuo vya
Ufundi, Utalii, Ujasiriamali, na Vyuo Vikuu: Tsh 20,000/=.
Mwisho
wa maombi : 14 April 2017
Viambatanisho
Barua iambatane na
·
Picha za rangi 5 passport size;
·
Vivuli/nakala za Maotokeo kila ngazi ya masomo kwa aina ya maombi ya
taaluma.
·
Ada ya Maombi au lisiti HALISI [original]
iliyolipia pesa Benk CRDB, Benki Akaunti 0152392952700, Jina la Akaunti Uhai
Tanzania, iliyotajwa juu. au PESA TASLIMU iletwe katika semina wakati wa kuomba
tu pamoja na barua ya maombi {HAKUNA FOMU ZA MAOMBI} na hakuna ada ya
kusajili, na hakuna mtihani
MUHIMU:
Kwanza
Watakao
someshwa chini ya Ufadhili huu, mbelini ndani ya mika 10 na
mingine 20 [yaani miaka 30 ya programu
hii] ijayo wengine watasoma Bure na wengine kwa punguzo kubwa sana na kwa manufaa zaidi.
MUHIMU:
Pili
Waombaji walio Dar es salaam wanatakiwa kuhudhuria
Shughuli za Uzinduzi wa kitaifa na
Kimataifa 4 March 2017.
Waombaji waliochaguliwa kuanza kusoma kutoka
Mikoani wataarifiwa kupitia vymbo vya habari na mawasiliano yaliyotumika
kuomba.
Pili huma za usafiri zitakuwa kwa mabasi ya Daraja
la Kati na daraja la Kwanza tu ya Makampuni ya Arusha One, Dar Express
[Arusha to Dar] , Dar Lux Tunduma, Mbeya , Kahama na Mwana –Arusha
Nairobi to Dar] , Shabiby [Dodoma to
Dar], NBS [Kigoma, Tabora to Dar], Tashirif,
Mining Nice, Superfeo [Songea, Iringa,
Njombe, Morogoro to Dar], Falcon [Tarime, na Mtukula- Bukoba Mwanza, Lusaka,
Harare,to Dar]. Ota High Class, Trinity,
[Kigali-Kagera-Dara],
Wazazi/waombaji wanaruhusiwa kupiga Simu 0714 41 81 90 kuulizia taratibu za jinsi ya kutuma maombi ili wasikwame. [Wanafunzi
wa SUA waliohudhuria Semina zetu June 2015 wanahimizwa Kuomba].
Sehemu ya pili ya Ufadhili ni Malipo ya Ada
Maalum. Wazazi wanaotaka kulipia sehemu ya Ada bila kuchujwa, Ada zipo
wawasiline nasi.
Wasicha wanaofanya kazi za ndani [housegirls],
waliokatisha masomo, walipata mimba na kuacha shule, wanaoshindwa kulipa karo, waliofeli
mitihani, waliokosa ufadhili, wanaosoma QT, wanaotoka familia bora , n.k wanaruhusiwa
kuomba ndani na nje ya Tanzania wanaruhusiwa kuomba. Wazazi wanaotaka kulipa ada
moja kwa moja waandike barua na waiambatanishe katika barua ya Mwanafunzi kuwa
wapewe nafasi za kulipa sehemu ya Ada Maalum yenye Punguzo a Ofa Kubwa].
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji,
Uhai Tanzania, Dar es Salaam, Makao
Makuu
0714418190;uhai1tz@yahoo.com ;
[Na 2B/2017DNMD]
0 comments:
Post a Comment