IFMSO Wizara ya elimu yafanikisha upatikanaji wa vimbweta vya kusomea chuoni (IFM) kwa udhamini wa Pepsi

Waziri mkuu serikali ya wanafunzi (Kulia) na raisi wa serikali ya wanafunzi (Kushoto) IFM wakipokea vimbweta vilivowasili kutoka pepsi, Jumapili ya tarehe 20/11/2016


SHUKRANI ZA DHATI KWENDA KWA KAMPUNI YA SODA (PEPSI)

Serikali ya wanafunzi IFMSO 2016/2017 chini ya wizara ya elimu inatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mzuri uliopata kutoka kwa wadhamini wao Pepsi kwa kuwapatia vimbweta vya kusomea (Kama vinavoonekana kwenye picha juu).

Ikiwa ni mwanzo wa kutimiza baadhi ya ahadi alizozitoa raisi wa serikali ya wanafunzi wa IFM Mh. Kilonzo Mringo pamoja na makamu wa raisi Mh. Justin laban wakati wa kampeni zao za kugombea uraisi "Kuboresha mazingira mazuri ya kusomea kwa wanafunzi wa IFM ".

Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Mh. Usama Mohamed alisema mbele ya vyombo vyetu vya habari kuwa atasimamia kadri ya uwezo wake ilani za raisi kutimia, na akaendelea kwa kusema vimbweta vilivofika ni vichache tu vipo vingine vipo njian na karibuni vitawasili chuoni.

Mwisho kabisa alipongeza jitihada kubwa na za makusudi zilizofanywa na kampuni ya Pepsi kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa serikali ya wanafunzi wa IFM na kuomba ushirikiano huo uzidi kudumu kwaajili ya maendeleo ya wanafunzi na umma wa Kitanzania kiujumla.


Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment