Taarifa ya maandamano ya amani chuo cha usimamizi wa fedha.




TAARIFA YA MAANDAMANO YA AMANI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA

Baada ya serikali ya wanafunzi kufikisha taarifa ya maandamano ya amani katika ngazi husika.
Serikali ya wanafunzi wa IFM kwa niaba ya wanafunzi wa IFM inatangaza maandamano ya amani yatakayofanyika siku ya Jumatano ya tarehe 22/3/2017.
Maandamano hayo ya amani yakiwa na malengo yafuatayo;
1. Kukemea matukio ya uvunjifu wa amani kwa wanafunzi na wanajamii waishio Kigamboni, kama vile kuporwa vitu vyao vya thamani, kuchaniwa madirisha, kuvamiwa na watu wenye silaha kali na kuwajeruhi na mpaka kufikia kuua.

2. Kuhamasisha umoja na ushirikiano kati ya wanajamii waishio kigamboni na wanafunzi katika kuimarisha ulinzi wao na mali zao.

3. Kukumbusha jamii kiujumla kuhusu jukumu lao la kushirikiana ipasavyo na vyombo vya usalama kutokomeza matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani katika maeneo husika kwa kutoa taarifa ya wahalifu hao punde tu wanapowashuku na kutoa msaada kwa jeshi la polisi wanapohitajika kufanya hivyo.

NB: Ikumbukwe ya kuwa, maandamno haya ni ya amani na hayaashirii kwa njia yeyote ile kusababisha uvunjifu wa amani wa aina yoyote.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI IFM
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

2 comments:

  1. Maandamano ya amani ya nini jamani, mbona serikali hii ya ifm-so ipo nyuma Sana kwenye idara nyingi tofauti na serikali shupavu zilizopita. Mimi ninavyoona tufanye msako kigamboni nzima juu ya hawa vibaka. Tukamate mateja na wahuni wote tuwape kichapo tuwadhibiti mpaka atapatikana mmoja atayetaja wenzake na mwishowe walioua wote tutawapata. Hii itakuwa fundisho Kwa wahuni wengine, watawaogopa kuwaibia wanafunzi na jamii nzima Kwa ujumla. Mimi nikimgundua katili aliyemuua mwanafunzi mwenzetu nitamtoa hata kichwa, pumbavu nitakula nyama yake na kumzika akiwa. mzima .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huoni kama unaingilia majukumu ya jeshi la polisi, na nikuulize. Je kufanya ivo kupo kisheria?

      Delete