(Kwa siti ya mbele kushoto kwenda kulia) Spika wa bunge, Waziri mkuu, Naibu spika na waziri wa mikopo IFM-SO
Registrar wa chuo, Raisi wa wanafunzi IFM-SO, Makamu wa raisi IFM-SO Kwa utaratibu.
TANGAZO KWA WANUFAIKA WA MIKOPO
Tunawatangazia wanufaika wote wa mikopo wa mwaka wa pili na wa tatu wenye allocations kuanzia asilimia moja hadi mia moja ambao wameona majina yao kwenye mbao za matangazo. Wanatakiwa kufika kwenye idara zao wakiwa na vitambulisho vyao (Vipya kwa wenye navyo na wasiobadilisha bado wafike na vitambulisho vyao vya zamani) na wataweza kusaini fedha zao za malazi na kujikimu.
Wafike siku ya ijumaa na jumamosi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni. Tunaomba wanufaika wote kuzingatia muda. Zitatumika siku mbili tu ili kuandaa malipo kwa haraka.
Wanufaika wote wenye allocations (waliomalizia ada na wasiomalizia ada) kwa mujibu wa registrar wapo registered na vitambulisho vyao vipo tayar. Watavikuta vitambulisho vyao vipya kwa wakuu wa idara zao na wataruhusiwa kusaini sharti tu uwe umefika na kitambulisho chako cha zamani, ila hawatoruhusiwa kuondoka na ivo vitambulisho vipya mpaka pale watakapomalizia kulipa madeni yao ya ada ndipo wataweza kupewa vitambulisho vyao vipya.
TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU KUFANIKISHA ZOEZI HILI.
WANUFAIKA AMBAO MATOKEO YAO YAPO BODI
Kwa wanufaika ambao matokeo yao yapo bodi ya mikopo, baada ya kikao kilichoitishwa na management ya chuo ikiwakilishwa na registrar, pamoja na viongozi wa IFM-SO (Raisi, makamu, waziri mkuu,ofisi ya bunge, mawaziri, wawakilishi wa vitivo na wawakilishi wa madarasa), management imeahidi kufuatilia kwa haraka allocations za malipo kwa wanufaika hao kurudi kwa wakati, pia serikali ya wanafunzi kupitia wizara ya mikopo iliahidi kuendelea kufuatilia bodi ili kushinikiza malipo hayo kufanyika kwa haraka. Kabla ya wiki ijayo kama allocations hizo hazitarudi chuoni, serikali ya wanafunzi itatoa msimamo wake.
Wizara ya mikopo
IFM-SO
0 comments:
Post a Comment