TANGAZO
Ni
haki ya kila mwanafunzi kutoa maoni,
kushauri au kuikosoa serikali ya wanafunzi ifm ili kujenga chuo cha ifm. Lakini mwanafunzi
ataruhusiwa kufanya hivi vitu
vitatu kwa nidhamu, busara na hekima. Hivyo basi kwa yeyote yule atakayeonesha utovu wa nidhamu kama vile
kutumia lugha chafu katika mitandao ya kijamii kama whatsapp dhidi ya serikali ya wanafunzi ifm-so hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Kwa sababu hiyo serikali ya wanafunzi (IFM-SO) ingependa kuwataarifu viongozi wote wa makundi ya
whatsapp( group admins) kuwa makini na wajumbe(members)
wao katika makundi yao hayo.Ikitokea mjumbe(member) yeyote kafanya utovu
wa nidhamu basi group admin atatakiwa kumuwajibisha mjumbe huyo kisheria. Kinyume na hivyo mkuu wa kundi atawajibishwa na serikali ya wanafunzi IFM-SO kamati ya nidhamu.
0 comments:
Post a Comment