Taarifa muhimu kwa wanufaika wote wa mikopo IFM .

NJOO USAINI ADA SEMESTER YA PILI

2015/2016 (BAC, BBF, & BTX)
Mwisho wa zoezi la kusaini ada semester ya pili ni kesho kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa kumi na moja kamili jioni, mbele ya Th. A na B.
Wahusika: Mwaka wa 1 mpaka wa 3
Kumbuka: Kitambulisho cha muhula wa pili mwaka wa masomo uliopita 2015/ 2016 kinahitajika. Mwanafunzi unaombwa kusaini bila ya kukosa hata kama ulisaini mwaka wa masomo uliopita unaombwa kusaini tena upya, vitabu vimefanyiwa marekebisho.

Majina ya wanufaika wanaoendelea na masomo waliokuwa na matatizo kwenye matokeo yao:
Majina hayo yasharudi chuoni na tunatarajia kuanza zoezi la kusaini kuanzia jumatatu ya tarehe 21/11/2016.

Wanufaika wasioona majina yao 
Wale wanufaika ambao majina yao hayajaonekana kati ya majina yaliyokuja wanaombwa kuwa na uvumilivu, majina yao yameonekana kuwa na matatizo na yanashughulikiwa. Takriban majina 226 hayajaonekana tunaomba muwe wavumilivu, tunawajali sana.

Wafuatao matokeo yao yanakosa sifa za kuendelea na mkopo, tafadhali shughulikia issue zako mapema kabla ya tarehe 20 Nov 2016, na kama kuna changes fika ofisi ya mikopo (Loan Officer) kwa taarifa zaidi.    BONYEZA HAPA KUYAONA MAJINA

Matokeo ya hawa wanafunzi yalitumwa awamu ya kwanza lakini Wanafunzi hawa hawakupata allocation, tunasubiri allocation kwa batch inayofuatia.  BONYEZA HAPA KUYAONA MAJINA

Wizara ya mikopo
IFM-SO  



Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment