Umoja wa vyuo 6 kutatua tatizo la makazi kwa wanachuo katika vyuo husika




Umoja wa mawaziri wa mambo ya nje (off Campus/ foreign/ external affairs) kutoka vyuo sita (6) (IFM, DMI, MAGOGONI, MWALIM NYERERE, CBE, & DIT) leo tarehe 08/09/2016 ndani ya chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) ikiundwa na Baraza la mawaziri, manaibu, pamoja na makatibu wa wizara za mambo ya nje (Off campus) wakishirikiana na wabunge/ wawakilishi maeneo kutoka Ferry, Kigamboni, Tuamoyo, Tungi, Muungano, Magomeni, K/koo, Magomeni, na kinondoni. Kwa umoja wao wakitambulika kama OCM (Off Campus Ministries) wamemteua Mh. Suka, Machomane J kutoka IFM kuwa mshikiliaji wa nafasi ya mwenyekiti wa umoja huo kabla ya uchaguzi rasmi.

OCM
Umoja wa wizara za off campus chini ya mwenyekiti teule Mh. Suka, Machomane J. Inapenda kutangaza utaratibu mpya ambao utanufaisha wanachuo na jamii nzima kwa ujumla. 

KWANZA
OCM wanapenda kuwatangazia wanavyuo wote (IFM, DMI, DIT, CBE, MWALIM NYERERE NA MAGOGONI) Kuwa imeanzisha mfumo wa kuwatafutia wanavyuo makazi kwa wote wanaotaka kukaa nje ya hostel za chuo husika.

NINI UNATAKIWA KUFANYA KAMA MWANACHUO?
Mwanachuo atahitajika kufika au kutuma muwakilishi wake(kwa wanafunzi walioko mikoani) kufika katika ofisi za serikali ya wanafunzi ( IFM-SO, MA-SO, COBE-SO, DIT-SO, DIM-SO, au TPSC-SO)na kuacha majina yake matatu, namba za simu, na ainishe anapotaka kwenda kukaa, pia abainishe kama anahitaji kukaa hostel au kuchukua chumba, na kama ni chumba aweke wazi ni cha peke yake au cha wawili.

MWISHO
Mwenyekiti wa OCM, akishirikiana na wajumbe wa maeneo, kila siku ya jumamosi mwenyekiti atawafikisha wanafunzi katika makazi waliyochagua. 

FAIDA ZA MFUMO WA KUWATAFUTIA WANACHUO MAKAZI
FAIDA KWA WANACHUO:
1)      Kuwalinda wanachuo wetu kutapeliwa na madalali wasiokuwa waaminifu.
2)      Kuepusha kero kwa wanachuo kudaiwa pesa za udalali na madalali wengine kuomba pesa mara mbili, kwa mwanachuo na kwa mmiliki wa hostel au vyumba.
3)      Kuwadhamini na kuwaombea wanachuo makazi. Endapo mwanachuo amekosa pesa ya kulipa kodi kwa wakati, OCM watakuwa wakiwaombea wanachuo wapatiwe makazi na wamiliki wa hostel au vyumba, pindi mwanafunzi atapata kodi atatakiwa kumlipa mmiliki kwa wakati.
4)      OCM itapata kutambua maeneo yanayokaliwa na wanachuo. Kamati nzima itakuwa ikifanya ziara katika maeneo ambayo inayatambua kwaajili ya kubaini matatizo katika maeneo hayo na kwa haraka kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo.
5)      OCM kupata taarifa kwa wakati endapo mwanachuo anaumwa, kaibiwa, anaonewa au kunyanyaswa, na kujua kero zifanywazo na wanachuo kirahisi.
6)      Kufufua uhusiano mzuri kati ya wamiliki na wanachuo, wanachuo na OCM, OCM na wamiliki, na kati ya OCM na serikali za mitaa.
7)      Kuwatafutia wanachuo makazi yenye bei nafuu, na OCM kufanya ukaguzi na upatikanaji wa umeme, maji, maliwato na sehemu za kusomea (Viti na Meza).
8)      Mwanachuo hatochajiwa chochote na kiongozi au mwanakamati yeyote, NI BURE. 

FAIDA KWA WAMILIKI
1)      OCM itawasaidia wamiliki kutodhulumiwa kodi zao na wanachuo.


WABUNGE/ WAWAKILISHI WA MAENEO (OFF CAMPUS)
S/N
JINA
NAMBA YA SIMU
ENEO
CHUO
1.
EMMANUEL I. NYAMSABA
0653 355 815
KIGAMBONI
IFM
2.
MWAWEZA WATSON GIDEON
0625 484 866
MAGOGONI
IFM
3.
ROMWARD ABEL
0712 994 423
MUUNGANO
IFM
4.
GODLISTEN MUSHI
0656 839 732
TUNGI
IFM
5.
HEMED YAHYA
0655 397 826
FERRY
IFM
6.
JOSEPH BONIPHACE
0688 028 382
TUAMOYO
IFM
7.
RUKIA MSEMWA
0766 817 568
KARIAKOO
TPSC
8.
VESTINA B. VEDASTO
0715 748 350
MAGOMENI
DIT
9.
ELIZABETH D. MELLECK
0659 118 411
KINONDONI
DIT
10.
HENRY A. JANE
0687 410 552
KINONDONI
DIT


NB:
-          Kuainishwa kwa chuo cha mbunge au muakilishi haina maana ya kuwa hawezi kutoa huduma kwa mwanafunzi tofauti na chuo chake.
-          Kumbuka huu ni umoja wa vyuo (6) (na kuna uwezekano wa kuongezeka). Ni jukumu la kila mmoja katika OCM kumhudumia mwanafunzi yeyote kutoka katika chuo chochote miongoni mwa vyuo sita mwenye shida inayohusu Off campus.
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

3 comments:

  1. Shukran sana serikali za wanafunzi za vyuo hivo husika kwa kusaidia hili. Kwa hakika litasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo ya wanafunzi

    ReplyDelete
  2. Hahaha..!! OCM wamecheza kama Messi, Mie nawatakia heri Mungu awaongoze mipango mliyo panga kuifanya na kuitimiza kwa ustadi zaidi.. Woow!! Hakika ni good Ideal eveeeer..

    ReplyDelete
  3. Hahaha..!! OCM wamecheza kama Messi, Mie nawatakia heri Mungu awaongoze mipango mliyo panga kuifanya na kuitimiza kwa ustadi zaidi.. Woow!! Hakika ni good Ideal eveeeer..

    ReplyDelete