TAARIFA KUTOKA OCM
OCM imefanikiwa kumaliza vikao vyake na ofisi za serikali za
mitaa kwa kata ya kigamboni na kata ya Tungi. Ikijumuisha wabunge au
wawakilishi wa maeneo na wamiliki wa Hostel na vyumba kwa kila ofisi ya
serikali ya mtaa.
Ofisi za serikali za mitaa ambazo OCM imefanikiwa kufanya
vikao navyo pamoja na wamiliki wa Hostel na
Vyumba ni Ferry, Kigamboni, Tuamoyo, Tungi, Magogoni na Muungano.
Hivyo basi, maazimio ya vikao hivyo ilikuwa kupata utatuzi
madhubuti wa suala la ulinzi na usalama kwa wanafunzi wenzetu na mazingira
wanayoishi kiujumla.
Kwa wamiliki wa Hostel wote kwa pamoja katika kata ya
Kigamboni na Kata ya Tungi, wanatakiwa kuweka walinzi private katika Hostel zote zikaliwazo na wanachuo.
Na kwa wanaoishi katika maeneo mbalimbali katika kata hizo
mbili, vilevile suala la ulinzi na usalama tutalisimamia kwa kushirikiana na
afisa mtendaji kata ya Kigamboni na Afisa mtendanji kata ya Tungi. Pamoja na OCD
kata ya Tungi. Pia tukishirikiana na ofisi za serikali za mitaa kutoa walinzi
shirikishi kwa kila eneo.
TANGAZO KUTOKA OCM
OCM inapenda kuwatangazia wanachuo wote wa IFM, CBE, DIT,
DMI, MA, & TPCS kuwa tunawaomba wanachuo wetu wasikae sehemu ambazo OCM
haitaweza kuwafikia, bali tunapendekeza wanachuo wakae sehemu ambazo
tunazitambua na ni rahisi kuwafikia.
Sehemu hizo ni:
KATA YA KIGAMBOMBONI:
i)
Ferry
ii)
Kigamboni
iii)
Tuamoyo
KATA YA TUNGI
i)
Tungi
ii)
Muungano
iii)
Magogoni
Na kwa wale wasiotaka kuishi Kigamboni, tutawatafutia makazi
katika sehemu zifuatazo:
i)
Kariakoo
ii)
Magomeni
iii)
Kinondoni
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI YA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO CHAKO
0 comments:
Post a Comment