PARLIAMENTARY COMMUNITY SERVICE.
Bunge la wanafunzi IFM, (ISRC 2016/2017) kwa kushirikiana na wizara ya ustawi wa jamii ya wanafunzi IFMSO wanakuletea tena mwanafunzi wa IFM nafasi ya kushiriki huduma ya kwenda kuwatembelea wagonjwa wenye magonjwa ya kansa na saratani tarehe 8.4.2017 (JUMAMOSI) katika kituo cha saratani Tanzania (Ocean road hospital) ambayo itaambatana na semina ya magonjwa hayo hapa chuoni IFM main cumpus siku hiyohiyo.Tuendelee kuchangia kwa ajili ya kuwawezesha ndugu zetu walio na uhitaji na hawawezi kutokana na magonjwa hayo.(dawa & nauli)
Kamati ya maandalizi itapita madarasani kwa ajili ya kuhamasisha, wawakilishi wa madarasa wanaendelea na zoezi la kukusanya michango, (kwa mwenye michango ampatie Cr wake)
Tujiandae kuwepo kwa wingi, tujifunze,ili kuisaidia jamii yetu juu ya magonjwa ya saratani, ili tuwe mabalozi wazuri wa kupambana na magonjwa ya saratani
Wagonjwa wananihitaji mimi na wewe. Jamii inakutegemea msomi uikomboe na janga hili kwa kuwaelimisha. Tuungane kwa pamoja kupata elimu, tuungane kuwapa moyo wagonjwa wa kansa
MGENI RASMI: MAMA ANE MAKINDA(MWENYEKITI WA MFUKO WA BIMA WA TAIFA)
MUDA: SAA 3:00 ASUBUHI-8:00 MCHANA.
VENUE: IFM MAIN CAMPUS.
MEDIA: CLOUDS
T-SHIRTS AVAILABLE TSH 13000.
Charity sees the need, not the cause
"let's walk with them through Cancer."Imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi.
Naibu spika- ISRC IFMSO
Selestina Mtorobo.
0 comments:
Post a Comment