TAARIFA KUHUSU FEDHA ZA FIELD KWA WANUFAIKA WALIOKO NJE YA DAR ES SALAAM
- Baada ya kikao cha Management ya chuo na Serikali ya wanafunzi kwa mara nyingine tena juu ya upatikanaji wa "field allowance" kwa wanufaika wa mikopo walioko mikoani.
- Management ya chuo imekubaliana na ombi la serikali ya wanafunzi (IFM-SO) kwamba itafanya malipo kwa wanafunzi hao ambao hawajasaini kwa kuzingatia matokeo yao (wale wenye matokeo yanayowaruhusu kuendelea na masomo kwa mwaka mwingine wa masomo wataingiziwa fedha hizo). Kwa mujibu WS management ya chuo, Fedha hizo zitaingizwa jumatano au alhamisi ya week ijayo (7 & 8/9/16). Utaratibu huo unafanyiwa kazi kwa haraka kama tulivoomba ili wanafunzi wapate pesa hizo mapema baada ya kupata maamuzi hayo kutoka kwa viongozi wa utawala wa chuo.
- Ikimaanisha kuwa, kwa wale waliokuwa discontinued na kushindwa kuendelea na masomo, hawataekewa fedha zao bila ya kusaini na itawalazimu kufika chuoni kwaajili ya kufuatilia suala hili.
0 comments:
Post a Comment