TAARIFA KUHUSU MAUAJI YA MWANAFUNZI WA IFM
Mnamo tarehe 12/03/2017 Siku ya Jumamosi mwanafunzi wa IFM anaetambulika kwa jina la HAMIS TWAHA aliekuwa akisoma mwaka wa pili kozi ya kodi ameuawa na vibaka (waendeshao pikipiki) kwa kuchomwa kitu cha ncha kali maeneo ya shingoni na kupoteza uhai wake papo hapo.
Tarehe 14/03/2017 IFM-SO pamoja na wanafunzi wa IFM wakishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu walisafirisha mwili kuelekea Tanga kwaajili ya kuupumzisha mwili wa mwanafunzi mwenzetu.
Maelezo juu ya picha hapo juu.
Serikali ya wanafunzi ikishirikiana na ofisi ya mlezi wa wanafunzi (Dean of student) wa IFM ilifika Kituo cha polisi siku kadhaa baada ya tukio na kukutana na Afisa upelelezi Kituo cha polisi kata ya kigamboni ili kupata mrejesho wa tukio zima lilivotokea na kutaka kujua hatua zilizofikiwa juu ya kuwapata wahalifu waliotenda kitendo hichi cha kinyama.
Majibu ya afisa upelelezi ni kuwa mara tu baada ya tukio kutokea, upelelezi ulianza na mpaka sasa wamefanikiwa kupata washukiwa kadhaa na kuahidi kutupatia taarifa kwa yoyote yatakayoendelea kujiri.
Vilevile serikali ya wanafunzi imewasilisha malalamiko juu ya matukio yanayoendelea kutishia amani ya wanafunzi wa IFM na wanafunzi wote kiujumla wanaoishi Kigamboni na kutaarifu polisi kuwa amani ya kigamboni kwa wanafunzi inatoweka na roho za wanafunzi zipo juu kuhofia usalama wao na vitu vyao.
Taarifa kwenda mamlaka husika ya ulinzi nchini:
Maeneo mengi ya kigamboni yamezungukwa na wanafunzi wa chuo cha IFM, Mwalim Nyerere, Magogoni, CBE, DIT, DMI, Muhimbili, TIA na Baadhi wa DUCE. Wanafunzi wanaosoma katika vyuo vyote hivi wamejawa na hofu katika nafsi zao juu ya usalama wao na mali zao baada ya matukio ya uvamizi na vibaka mpaka kufikia kuuawa.
Kauli mbiu ya nchi ni kuongeza idadi ya wasomi nchini, wasomi wenyewe ndio hawa kwa sasa wanashindwa kuwa na mazingatio mazuri katika masomo yao kwa kuhofia mda wowote, na siku yoyote kuvamiwa na vibaka wenye silaha kali.
Wanafunzi tunahitaji amani, usalama na utulivu ili kuweza kufikia malengo yetu yaliyotuleta vyuoni. Tunaomba mamlaka husika ya ulinzi kutilia uzito jambo hili na haraka kuweza kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hili.
Serikali ya wanafunzi
IFM-SO (2016/17)
0 comments:
Post a Comment