hitilafu ya umeme ndani ya chuo cha IFM

HITILAFU YA UMEME NDANI YA CHUO

Serekali ya wanafunzi IFM-SO kupitia wizara ya ulinzi na majengo inapenda kuomba radhi wanafunzi kwa tatizo la kutokuwepo kwa umeme madarasani kwa mida ya usiku, sababu kuu ikiwa ni hitilafu kutoka TANESCO. 

Chuo kimekua kikitumia umeme wa jenereta kwa siku nzima kutokea siku tatizo hili limeanza. Kutokana na jenereta la chuo kutumika kwa muda mrefu wakati wa mchana wanafunzi wawapo darasani kwaajili ya taa na viyoyozi, linakuwa linazidiwa nguvu na kupelekea mida ya usiku kupumzishwa na kuachwa umeme ndani ya hostel za wanafunzi na kuzima madarasani. 

Uongozi wa chuo unaendelea kushughulikia suala hili na karibuni tu huduma ya umeme itarudi kama kawaida na kuondoa changamoto iliopo.


Imetolewa na wizara ya majengo na ulinzi,
IFMSO 2016/17

Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment