TAARIFA YA YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA BODI YA MIKOPO
Kwa niaba ya wizara ya mikopo, Raisi
wa serikali ya wanafunzi IFM-SO alifanikiwa kuhudhuria mkutano wa ufafanuzi wa
mikopo ulioandaliwa na mkurugenzi wa BODI ya Mikopo tarehe 30 Oktoba 2016. BODI
imesema kuwa mwaka huu inatarajia kutoa Mikopo kwa jumla ya wanafunzi wapya
25,000 na mpaka Sasa imetoa kwa wanafunzi wapya 20,000 na kubakisha
nafasi 5,000 kwa watu watakao kata rufaa na watu wenye mahitaji maalumu.
Raisi wa wanafunzi aliuliza
yafutayo:
i) Swali: Kuna
wanafunzi wanaoendelea 53 katika chuo cha usimamizi wa fedha ni yatima na wapo
wenye maisha magumu na hawajapata mkopo Hali ya kuwa nao ni kipaumbele?
Jibu:
Wanafunzi hao wanatakiwa kukamilisha taarifa zao na
kuziwasilisha kwa waziri husika wa mikopo wa serikali ya wanafunzi kwa kuwa
hili ni suala la kiutawala watalishughulikia.
ii) Swali: Je!
BODI inataarifa juu ya suala la majina ya mwaka jana ya allocations
yanayosambaa katika mitandao ya kijamii na kuhusishwa na zoezi la kujaza taarifa
za kifedha kwenye akaunti za wanafunzi za BODI ya Mikopo?
Jibu:
Taarifa hizi ni za kizushi, BODI hawajatoa majina ya
namna hiyo na majina yote ya WANUFAIKA
wapya wa Mikopo yapo katika tovuti ya BODI ya Mikopo wanafunzi watembelee kwenye
tovuti.
iii) Swali:
Kwanini wanafunzi waliotokea diploma hawajapata mkopo?
Jibu:
Suala hili ni la kiutawala kwavile tumelifikisha BODI
litashughulikiwa. (tumemuagiza waziri wa mikopo IFM kulifuatilia).
iv) Swali: Kwanini
wanafunzi wanaoendelea kufanyiwa uhakiki wa kifedha kupitia akaunti zao za BODI
walizoombea na Kuna baadhi ya wanafunzi wanaweza kupoteza sifa za kupokea mikopo
hiyo kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na mkurugenzi wa BODI ya Mikopo, Je
hawaoni kama wanawanyima haki ya kimsingi wanafunzi ambao tayari walikua
wameingia mkataba Na Bodi ya mikopo?
Jibu: kila baada
ya kipindi flani kupita serikali hufanya uhakiki wa wanufaika wa mikopo kwaajili
ya kuboresha mifumo yao ya utoaji wa mikopo hiyo.
Raisi akaendelea
kuhoji: kwanini mifumo hii isitumike kuanzia mwaka huu wa masomo na
kuendelea maana vigezo vya mwaka Jana havifanani na mwaka huu. (mwaka Jana Kuna
wanafunzi walipata mkopo kwa sababu ya ufaulu wao kuwa mzuri).
Maoni ya Raisi:
Kwa upande wetu sisi bado tunaona BODI ya Mikopo Kuna haja ya kulifanyia
tathmini upya suala hili ili lisiwaathiri wanafunzi wengi kisaikologia na
kujiingiza kwenye vitendo viovu, tunaisihi sana BODI ya Mikopo kuliangalia upya
suala hili ni mategemeo yetu kuwa litafanyiwa kazi.
v) Swali: Kwanini
Kuna poromoko la WANUFAIKA wapya wa mikop mwaka huu kulinganisha na mwaka Jana
ambapo tulikua na WANUFAIKA zaidi ya 40,000 Lakin saivi ni WANUFAIKA 25,000 tu?
Jibu:
Sio walioomba wote mwaka huu wanasifa za kupewa Mikopo,
waliopewa mikopo ndio wanasifa za kupokea mikopo hiyo.
vi) Swali: Katika
kujaza taarifa za kifedha kwenye akaunti za wanafunzi walizoombea mkopo wapo
waliosahau neno la siri (Password), wanasaidiwaje?
Jibu:
BODI watatoa utaratibu kuanzia Jumatatu juu ya namna
gani hao wanafunzi wafanye ili waweze kuingia kwenye akaunti zao.
RAI YA RAISI WA
IFM-SO KWA WANAFUNZI WA IFM
Raisi anaomba wale wenye mahiitaji maalum hususan
mayatima wafikishe taarifa zao kwa wizara ya mikopo kuanzia kesho (31/10/2016) ili tuwasihi BODI wawatambue wanafunzi hao wenye hali ngumu ya kimaisha lakini kwa wanaondelea wote wawe na mshikamano na kutusikiliza viongozi wenu
tutaendelea kusimamia haki zenu kwa nguvu zetu zote.
Pia tunataraji kupokea vitabu vya WANUFAIKA wa Mikopo
wanaoendelea hivi karibuni ili watu
wasaini meals and accommodation.
Je! Unahitaji mkopo wa haraka ili uondole deni lako au unahitaji mkopo wa usawa ili kuboresha biashara yako? Umekataliwa na mabenki na mashirika mengine ya kifedha? Je! Unahitaji uimarishaji wa mkopo au mikopo? Utafute tena kama tuko hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani.
ReplyDeleteHii ni kampuni rahisi ya mkopo. Tunatoa mikopo kwa wale wanaopenda kiwango cha riba cha 2%. Mipangilio mbalimbali kutoka $ 5,000.00 hadi dola za dola 100,000,000.00.
Mikopo yetu ni bima nzuri kama usalama wa juu ni kipaumbele chetu.
Wasiliana nasi kwa barua pepe: oceanfmortgages@gmail.com
Uzidi
Max Bent
oceanfmortgages@gmail.com
Mikopo ya 2% ya awali na dhamana
oceanfmortgages@gmail.com