Maendelo ya Aileen, Hospitali ya Muhimbili

MAENDELEO YA MGONJWA WETU AILEEN ALIOKO MUHIMBILI

Jana tarehe 26/08/2016 mnamo mida ya saa 10 jioni, serikali ya wanafunzi (ikiongozwa na ofisi ya raisi, ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya spika wa bunge) pamoja na wanafunzi wa IFM, ilifika hospitali ya taifa ya muhimbili kwaajili ya kumuona mgonjwa mwanafunzi mwenzetu.
Hali ya mgonjwa hapo jana haikuwa nzuri ukilinganisha na leo 27/08/2016, kwani hakuweza kufumbua macho, bali leo asubuhi baada ya serikali ya wanafunzi kufika hospitali imekuja na taarifa za kutupa moyo kuwa mgonjwa wetu ameweza kidogo kufumbua macho na kugeuza geuza mwili wake.
Serikali ya wanafunzi IFM-SO ilifanikiwa pia kuonana na mama mzazi wa mgonjwa na kutoa pole kwa mama kwa uuguzaji vilevile kuahidi ushirikiano na familia ya mgonjwa kwa hali na mali.


Zingatio:
Hali ya mgonjwa bado haijatengamaa, anahitaji sana dua zetu na michango yetu ya hali na mali (kumuona mgonjwa vilevile kuchangia tulivyonavyo ili kufanikisha gharama za matibabu zinazoendelea kutumika kila siku). Wana IFM wote ni wamoja, tatizo la mmoja wetu ni tatizo letu sote, tuguswe na hili na tuhisi kuwa Aileen anamuhitaji kila mmoja wetu.


Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment