Taarifa kwa wanufaika wa mikopo mwaka wa kwanza na wanaoendelea IFM

TAARIFA KWA WANUFAIKA WA MIKOPO

Wizara ya mikopo IFM-SO inapenda kuwataarifu kuwa juhudi zetu tukishirikiana na waziri mkuu(Baada ya kuzuia wanafunzi wasisaini vitabu vilivyoletwa kwa mufuata viwango vya mean tested na kuishawishi bodi na serikali kuongeza idadi ya wanufaika pamoja na kurudisha viwango (pesa) vya kawaida) hatimaye zimezaa matunda kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao pesa zao za kujikimu pamoja na books and stationary zilikuwa zimewekwa kwa viwango vya mean tested na pia kutoka kwa majina machache ya wanufaika kwa mwaka wa kwanza.

Kufikia sasa majina ya wanufaika wa mwaka wa kwanza 2016/2017 yamefikia 401 na pia viwango vya utoaji pesa za kujikimu vimerudishwa katika hali yake ya kawaida. Pamoja na hayo tunafurahi pia kila mwanafunzi amepata mkopo asilimia 100, lakini bado juhudi zinaendelea kufanyika idadi ya wanufaika iongezeke maradufu pamoja na wanafunzi wanaoendelea walioomba mkopo wapate mkopo kwa idadi kubwa.

WANUFAIKA WANAOENDELEA (CONTINUING STUDENT)

Ofisi ya mikopo inafuatilia kwa ukaribu pesa za ada na za kujikimu, wanafunzi mnaombwa kuwa na uvumilivu na kuendelea na masomo kama kawaida. Wenye status ya PRIVATE na ni mnufaika asiwe na wasiwasi allocation zikifika status itabadilika.


IMETOLEWA NA SERIKALI YA WANAFUNZI (IFM-SO)
WIZARA YA MIKOPO

 

Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment